ESTHER GITHUI EWART

Printer-friendly versionPDF version

Esther Githui Ewart ni mtangazaji katika idhaa ya Kiswahili na televisheni ya Sauti ya Amerika. Ni mzaliwa wa Kenya ambaye alisomea uandishi habari katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Kabla ya kujiunga na chuo hicho alisomea shahada ya elimu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta na kufundisha kwa muda mfupi katika shule mbalimbali za sekondari nchini Kenya . Anafahamika vyema nchini humo ambapo kwa muda wa miaka minane aliandaa vipindi na kusoma taarifa za habari katika Shirika la Utangazaji la Kenya (K.B.C.) kitengo cha televisheni na radio. Esther alijiunga na Sauti ya Amerika mwaka 2000. Mbali na kazi za kila siku za kuandaa ripoti na taarifa za habari, ni mhariri na mwandalizi wa kipindi kinachopendwa sana “Jarida la Jumapili” ambapo huwaletea mahojiano ya kina ya kijamii, kisia+sa kiuchumi na kitamaduni

UoN Website | UoN Repository | ICTC Website


Copyright © 2019. ICT WebTeam, University of Nairobi